Suala la mawasiliano ni muhimu sana katika maisha ya mwanadamu kwani hutuwezesha kupeana taarifa za kile kinachoendelea katika mazingira yanayotuzunguka hali kadhalika humuwezesha mtu kueleza kile anachofikiria. Kutokana na umuhimu wake ndio maana kwa sasa tunashuhudia maendeleo katika sekta hii (Information and Communication Technology development) yote ni kwa lengo la kufanikisha mambo hayo kufanyika kwa haraka zaidi.
Zaidi ya hapo, mawasiliano yanatuwezesha kujenga mahusiano mazuri kati yetu (socialization), kujenga uaminifu na haiba (trust & personality) ya mtu, pia hufanya watu kuvutiwa na kile tunachokifanya iwe ni biashara au huduma tunayoitoa kwa jamii (build customer interest) na kwa umuhimu wake ndio maana vitengo vya mawasiliano na huduma kwa wateja vikawepo katika sehemu nyingi za kazi. Yote haya yatafanikiwa endapo mzungumzaji atazingatia msingi ya uzungumzaji kama uchaguzi mzuri maneno kulingana na muktadha aliopo na kuangalia anazungumza na nani? (Choice of words according to context and your addressee). Kikubwa zaidi ni kukumbuka “body language” kama gesture, postures and our facial expression kwani hivi vinatoa tafsiri kubwa kuliko maneno tunayoyazungumza. Unaweza ukazungumza maneno yenye msingi bali body language ikayafanya yaonekane hayana msingi,kwani always body speaks than words
Kumbuka mawasilano yanaweza kujenga haiba na uaminifu mtu na kwa upande mwingine inaweza kuharibu haiba yako (destruct your reputation) endapo utashindwa kutumia vizuri. Communication is more than what we speak from our mouth. As a young communicators (PRs’) we have to know how to communicate with your audience.
For more just click and watch the slideshow of what we speak without words
Prepared by Bonnie Jacob